
Watu 14 waliokuwa kwenye ndege ya abiria, wamepoteza maisha baada ya ndege hiyo kuanguka nchini Sudan Kusini, baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Yei, kuelekea jiji kuu Juba.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ndege hiyo ndogo aina ya Cessna 208 inayomilikiwa na kampuni ya CityLink Aviation ilianguka takriban kilomita 20 kusini-magharibi mwa mji mkuu, Juba, Jumatatu asubuhi,baada ya udhibiti wa trafiki wa anga kupoteza mawasiliano takriban dakika 30 baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Yei.
Miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni rubani na abiria 14 , 13 wakiwa raia wa sudan kusini na Wakenya wawili.
Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa ajali hiyo huenda ilisababishwa na hali mbaya ya hewa, hasa kutoonekana vizuri,wakati huu kikosi cha kuchunguza ajali za ndege kikitumwa kwenye ĂȘneo la ajali hiyo kwa uchunguzi zaidi .
Katika kipindi cha muongo mmoja Zaidi ya ndege 55 zilianguka nchini humo na kusababisha vifo vya watu kadhaa nyingi za ajali hizo zikisababishwa na hali mbaya ya hewa na hali duni ya kuratibu safari za ndege nchini humo.