Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutekeleza mageuzi ya elimu nchini, timu ya Benki ya Exim ikiongozwa na Ofisa Mkuu wa Fedha, Shani Kinswaga imefanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda jijini Dodoma.
Timu hiyo wakiwamo Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wa kati Andrew Lyimo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Stanley Kafu imefanya kikao leo Jumanne Aprili 28, 2026 kikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Benki ya Exim.
Majadiliano hayo yalijikita katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya elimu, zikiwemo fursa za ufadhili wa wanafunzi wa elimu ya juu hususan wanaosomea sayansi ya data (Data Science), akili unde (Artificial Intelligence) na sayansi shirikishi.
Pia, mazungumzo hayo yaliangazia fursa mbalimbali ikiwemo ufadhili unaoweza kutolewa na benki hiyo, hususani kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaochukua masomo ya sayansi ya elimu ya data na akili.