Dar es Salaam. Baada ya kupindua ardhi juu chini na Chemsha Bongo. Hapo akiwa na kundi la Hard Blasters, ikiwa ni mwaka 2000. Mwamba sasa akaamua kutoka na albamu yake akiwa ‘solo atisti’. Machozi Jasho na Damu namuogelea Jay Profesa 

Katika albamu hii Pro. Jay alitoa shavu kwa wasanii kibao. Kama  Black Rhino, Adili Chapakazi, AY, Jide, Juma Nature, Babu Ayubu, Jaymoe, Complex, Imam Abbas na wengineo. Wengi walikuwa ni wapya likawa jukwaa lao rasmi la kuwatoa kisanii.

Lakini ukiachana na wingi wa wanamuziki. Pro. Jay aliweka rekodi yake ambayo huenda hata leo ikawa haijavunjwa. Mwamba alitoa ‘singo’ tano na ngoma hizo zote zilikamata namba moko. Ni katika chat zote za redio Bongo.

Singo za Jay,  karibu zote hizo zilijulikana sana kuliko wasanii kibao. Yaani nyimbo zilikuwa ni maarufu kuliko umaarufu wa wasanii wengi waliokuwepo kwa wakati ule. Hii rekodi haivunjwi kwa miaka hii kutokana na dunia inavyotaka.

Alianza na Bongo Dar es Salaam. Baadaye akaachia Jina Langu. Akaja na “Nawakilisha” ndani AY, Rhino, Complex, Adili Chapakazi humo waliua sana. Wakati huu ilikuwa ni dili kufanya ‘kolabo’ na Profesa Jay, kila aliyepewa shavu alishaini’. 

“Ndiyo Mzee” ikawa funga kazi hii. Ndani kuna Juma Nature na Jide. Na kibwagizo cha Babu Ayub pale mwanzo pini likiwa linaanza. Hii ngoma pia ilitikisa sana nchi. Kisha akatutuliza na pini mahaba la kuitwa “Mamsap” ndani wapo Hard Blasters. 

Akatupa ñini la “Tathimini” akiwa na Jaymoe. Zote hizi zilitoka kwa wakati usiopishana sana zikiwa kama singo za kuuzia albamu yake. Alikuwa hashikiki Jay kila pini lilifunika chati zite za redio kwa wakati ule. Kuanzia mjini Daslama mpaka mikoani. 

Jay amelihudumia taifa kupitia muziki wake, kwa miaka mingi sana. Tuzo aliyopewa jana siyo tu ni heshima kwa Profesa Jay, bali ni kwa muziki kwa ujumla. Kama tukiwa wakweli Jay anaudai huu muziki pesa nyingi sana. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *