
Marekani mwishoni mwa juma lililopita imetaka kuachiwa kwa wafungwa wote wa kisiasa nchini Sudan Kusini ndipo iweze kutoa msaada wowote wa kifedha kusaidia nchi hiyo kufanya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa Kidemokrasia baadae mwaka huu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Akizungumza siku ya Ijumaa katika kikao cha baraza la usalama la umoja wa Mataifa, balozi wa Marekani Mike Waltz, amesema majadiliano ya kweli hayawezi kufanyika wakati viongozi wakuu wa upinzani wako kizuizini, akiwataka raia amba oni walipa kodi kutofadhili mchakato wa kisiasa ambao serikali yao wenyewe imeshindwa kuufadhili.
Waltz amesema mkataba wa amani wa mwaka 2018 unapaswa kuheshimiwa, akisisitiza kuwa msaada wa nchi yake kwa uchaguzi wa nchi hiyo, utategemea ikiwa viongozi watatenga fedha za ndani kufadhili uchaguzi huo.
Akinukuu ripoti ya katibu mkuu kuhusu hali ya kisiasa nchini Sudan Kusini, balozi Waltz alisema ni wazi kuwa kwa hali ya sasa taifa hilo haliwezi kufanya uchaguzi, huru, haki na wakuaminika, wakati mmoja wa wanasiasa wakuu wa upinzani nchini humo akiendelea kuzuiliwa na kukabiliwa na kesi ya uhaini.
Kauli ya Marekani ilifuatia kupitishwa kwa azimio lililowasilishwa na Washington, ambapo nchi wanachama ziliridhia kuongeza mud awa mwaka mmoja zaidi kwa tume yake ya kulinda amano nchini humo, UNMISS.