Nchini Mali, kundi la Azawad Liberation Front (FLA) linalotaka kujitenga na kujitawala Kaskazini mwa Mali, linasema sio kundi la kigaidi, kama linavyotambuliwa na serikali ya kijeshi jijini Bamako, baada ya kuongoza mashambulizi ya Aprili 25.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa kundi hili, wanasema wao ni vuguvugu la kisiasa, linalotaka mageuzi muhimu ya utawala katika nchi hiyo ambayo inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya kiusalama.

Msemaji wa kundi hili Mohamed Elmaouloud Ramadane, anasema FLA lina mpango wa kuhakikisha kuwa wakaazi wa jimbo la Azawad wanajitawala na kuachana na utawala wa Bamako, ambao wanasema kwa miaka mingi umekuwa ukiwabagua na kuwatesa.

Ramadane, anaongeza kuwa FLA haiwalengi raia kama ilivyo kwa jeshi la Mali, ambalo anasema linaendeleza ushirikiano na mamluki kutoka Urusi, kuwashambulia wananchi.

Hata hivyo ripoti zinasema, wapiganaji wa kundi hilo wanashirikiana kwa karibu na kundi la kijihadi la JNIM, ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi dhidi ya wanajeshi, raia na hata kuwateka nyara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *