
“Mlipuko” uliofuatiwa na moto umekumba meli ya Korea Kusini katika Mlango wa Hormuz leo Jumatatu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini imetangaza, ikiongeza kuwa hakukuwa na majeruhi ndani ya meli hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Karibu saa 2:40 usiku huko Seoul, “mlipuko uliofuatiwa na moto ulitokea ndani ya meli iliyokodishwa na kampuni ya meli ya Korea Kusini, iliyotia nanga katika maji karibu na Falme za Kiarabu, katika Mlango wa Hormuz,” wizara imesema katika taarifa. “Sababu za mlipuko na moto huo, pamoja na kiwango sahihi cha uharibifu, kwa sasa zinachunguzwa,” wizara imeongeza.
Meli husika, HMM Namu, ni meli kubwa ya mizigo yenye urefu wa takriban mita 180, ikipeperusha bendera ya Panama, kulingana na data kutoka kwa tovuti ya MarineTraffic.
Wakati huo huo televisheni ya serikali ya Iran imeripoti kwamba wanajeshi wa jeshi la majini la Iran wamerusha makombora dhidi ya meli za kijeshi za Marekani katika Mlango wa Hormuz.
Jeshi la wanamaji la Iran limezindua mashambulizi ya makombora, ikiwa ni pamoja na makombora ya Cruz, kama onyo dhidi ya meli za kijeshi za Marekani katika Mlango wa Hormuz, televisheni ya serikali imeripoti, ikinukuu taarifa ya kijeshi.
“Meli za Marekani na Israel baada ya kupuuza onyo letu la awali, jeshi la wanamaji… lilizindua makombora ya Cruz, roketi, na ndege zisizo na rubani za kivita dhidi yao,” chanzo hicho kimesema.
Iran ilionya mapema kwamba itashambulia jeshi la Marekani ikiwa litakaribia mlango wa kimkakati, baada ya Donald Trump kutangaza mpango wa kusaidia meli zilizokwama kwa miezi miwili katika Ghuba.
Hata hivyo jeshi la Marekani limekana kwamba moja ya meli zake ilishambuliwa na Iran katika Mlango wa Hormuz, kama ilivyodaiwa na chombo cha habari cha Iran.