Nchi ya Falme za Kiarabu imekanusha madai ya Sudan kuwa, ndege zake zisizokuwa na rubani zilishambulia uwanja wa ndege wa Khartoum, siku ya Jumatatu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Sudan inasema ndege zilizoshambulia uwanja wake wa ndege, zilirushwa kutoka Ethiopia, ambayo ilishirikiana na Falme za Kiarabu kutekeleza shambulio hilo.

Tangu kuanza kwa vita kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF mwaka 2023, Sudan imeendelea kuishtumu nchi ya Falme za Kiarabu kwa kuwapa msaada wa silaha, RSF. Hata hivyo, nchi hiyo imekuwa ikikanusha madai hayo.

Ethiopia nayo imekataa tuhuma hizo za Sudan ambayo inasema iko tayari kujibu mashambulizi hayo iwapo yataendelea kushuhudiwa.

Nchi za Misri na Saudi Arabia ambazo zimeanza tena safari za ndege kuelekea Khartoum, zimelaani kushambuliwa kwa uwanja wa ndege wa Khartoum.

Massad Boulos, mshauri wa rais wa Marekani Donald Trump kuhusu masuala ya Afrika, amesema Sudan kuendelea kushambuliwa kutoka Ethiopia ni jambo linapaswa kukoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *