Rais wa Marekani Donald Trump amesema vita nchini Iran, huenda vikakamilika kwa upatikanaji wa mkataba, lakini anaonya kuwa, vita vipya vitaanza iwapo mkataba huo hautapatikana.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia mitandao yake ya kijamii ya Thruth, Trump amesema iwapo Iran itakataa makubaliano, jeshi la Marekani, litaanza kuishambulia tena.

Aidha, Trump ametishia kuwa mashambulizi haya mapya, yatakuwa ya kiwango cha juu, tofauti na ilivyoshuhudiwa hapo awali.

Kauli hii ya Trump imekuja, baada ya Waziri wake wa Mambo ya nje Marco Rubio, kusema kuwa mashambulizi mazito dhidi ya Iran yalikuwa yametamatika.

Aidha, Trump alikuwa ametangaza kuwa Marekani ilikuwa inasitisha operesheni ya kuzisindikiza meli za mizigo katika mlango wa Bahari wa Hormuz.

Wakati hayo yakijiri, ripoti kutoka Pakistan zinaeleza kuwa, jitihada za mazungumzo kati ya Tehran na Washington zinaendelea ambapo pande hizo mbili zinaelekea kukubaliana kuhusu pendekezo la ukurasa mmoja wa namna ya kusitisha vuta hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *