Mahakama ya Juu nchini Afrika Kusini, imebadilisha uamuzi wa bunge uliokuwa umesitisha mswada wa kumwondoa madarakani rais Cyril Ramaphosa, kwa tuhuma za ufisadi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ramaphosa anatuhumiwa kuwaficha polisi na mamlaka ya utozwaji ushuru, kuhusu Dola Milioni 4 fedha taslimu, zilizopatikana katika makaazi yake ya kafahari ya Phala Phala, Kaskazini mwa mkoa wa Limpopo.

Baada ya ugunduzi huo, uchunguzi huru ulibaini kuwa, huenda alikuwa amepata fedha hizo kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Ramaphosa amejitetea kwa kusema kuwa fedha alizokuwa nazo ni Dola za Marekani 580,000 baada ya kuuzwa nyati 20 kwa mfanyabiashara wa Sudan.

Licha ya ripoti hiyo, mwaka 2022 bunge ambalo linatawaliwa na chama tawala ANC kilikataa kuendelea na mjadala wa mswada wa kukosa imani naye.

Mahakama ya Katiba, kupitia Jaji wake Mandisa Maya, amesema hatua ya wabunge ilikuwa kinyume cha Katiba, na kuongeza kuwa ripoti hiyo iwalishwe tena kwa Kamati ya bunge, iliyokuwa inajadili mswada wa kukosa imani na rais Ramaphosa.

Uamuzi huu umekuja, baada ya chama cha upinzani cha EFF kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa wabunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *