
Nchini Rwanda, mkosoaji wa serikali, Aimable Karasira aliyefungwa jela amefariki dunia kutokana na matumizi ya dawa kupita kiasi siku ya kuachiliwa kwake, wakuu wa magereza wamesema.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Karasira, Mhadhiri wa zamani katika Chuo Kikuu cha Rwanda, aliikosoa serikali kwenye chaneli yake ya YouTube hali iliyosababishwa kukakamatwa mwaka wa 2021.
Karasira aliyenusurika katika mauaji ya kimbari, alishutumu Jeshi la Wazalendo la Rwanda RPA kwa kuwaua watu wa familia yake mara tu baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi.
Mahakama Kuu ya Nyanza Chemba ya Uhalifu wa Kimataifa na Mipaka ilimhukumu Septemba 2025 kifungo cha miaka mitano jela kwa madai ya kuchochea migawanyiko, ingawa alikuwa gerezani tangu 2021.
Ikithibitisha kifo hicho, Idara ya Marekebisho ya Rwanda ilisema Karasira alipelekwa hospitalini baada ya kutumia zaidi ya kiwango kilichopendekezwa cha dawa alizoagizwa na daktari wake.
Wakili wake ametaka uchunguzi huru ufanyike na wahusika kuwajibikaji huku akisema kifo hicho ni doa kwa sifa ya serikali.