
Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya harakati ya Hamas huko Gaza, amethibitisha kuuawa shahidi mwanawe, Azzam na rafiki yake, akisisitiza kuwa: Adui Mzayuni hawezi kupata maafikiano kwenye meza ya mazungumzo kwa kulenga na kuua familia zetu.
Khalil al-Hayyah amesema katika majlisi ya maombolezo ya mwanawe aliyeuawa shahidi na askari wa Israel, Azzam kwamba: “Ikiwa adui Mzayuni anadhani kwamba kwa kuwalenga viongozi, watoto wao wa kiume au familia zao, anaweza kuchukua au kufikia chochote anachotaka, amekosea mahesabu yake.”
Khalil Al-Hayyah ameongeza kuwa: “Dira yetu ni maslahi ya watu wetu na kufikia malengo yao halali ya kisiasa na yanayowawezesha kubaki imara na kutoyumba katika ardhi na nchi yao.
Al-Hayyah ameeleza matumaini kwamba hatimaye watu wa Palestina watapata ushindi, na heshima na fahari ndio njia yao; na dhulma na ukandamizaji hatimaye vitatoweka.