Msemaji wa zamani wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) amefichua kuwa: Majenerali waandamizi wa jeshi la nchi hiyo wana hofu kubwa kuhusu kuzungumzia vita vya maafa dhidi ya Iran.

John Kirby, msemaji wa zamani wa Pentagon, amethibitisha kuwepo mzozo mkubwa ndani ya jeshi la nchi hiyo na kusema: Majenerali waandamizi wana hofu ya vita dhidi ya Iran. Ameongeza kuwa: Serikali ya Donald Trump imewalazimisha kunyamaza kimya kabisa kwa kuwatishia kuhusu mafao yao ya kustaafu.

Wakati huo huo, matokeo ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Ujerumani ya Bertelsmann yanaonyesha kuwa, asilimia 73 ya raia wa Ulaya wanaamini kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kujitenga na Marekani, kufuata njia yake wenyewe, na kutenda kwa kujitegemea.

Aidha, asilimia 58 ya raia wa Ulaya hawaioni Marekani kama mshirika anayeaminika wa Umoja wa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *