#HABARI: Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imesema inaandaa mkakati maalum utakaomsaidia mfanyabiashara wa Tanzania anayeuza Biashara yake nje ya nchi kufanya biashara bila vikwazo vyovyote vya kibiashara, huku akiwataka watendaji waliochini ya wizara hiyo kuacha tabia ya kuwadhibiti wafanyabiashara hao na badala yake wawasaidie ili kuweza kunufaika na soko la nje.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kuwajengea uwezo Wafanyabiashara wa Tanzania, ili waweze kutumia fursa ya kuuza bidhaa zao nchini china bila kulipa ushuru.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya watu wa china nchini, Mhe. Chen Mingjian, akiongelea fursa mbalimbali zitakazopatikana kwa wafanyabiashara wa Tanzania nchini China Pamoja Wafanyabiashara wanaofanya biashara nchini china, ambapo pia mkutano huo uliandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China, ukihusisha viongozi wa serikali, sekta binafsi, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa kibiashara ulikuwa na lengo la kujadili namna ya kuongeza mauzo ya wafanyabiashara wa Tanzania katika soko la China.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)