Dar es Salaam: Ujue Miaka hii mambo ni rahisi rahisi sana. Yaani unaweza fika Posta, Moroko, Kariakoo, Pugu na Mbagala bila kushuka. Yaani ukipanda mwendokasi tu wewe unazunguka maeneo yote hayo kama mtalii wa Kitaliano mitaa ya Forodhani Zenji.
Siku hizi kila sehemu kuna pisi kali kali tu. Unaweza kutulia tu mitaa ya Mabibo Makutano. Na ukaopoa dem mkali ambaye zile enzi zetu ungekutana naye kule Upanga au Masaki. Dem yupo Vingunguti ndani ndani lakini ana ‘klasi’ ya Mikocheni.
Zamani dem mkali sana huwezi kukutana naye Ubungo Maziwa. Wengi waliishi ushuani Mbezi ya Beach, Kawe Beach, Msasani au Sea View. ‘Nau deizi’ wamejaa kila kona kuanzia Mpigi Majohe mpaka Msakuzi na Mwanagati au Kinyerezi ndani ndani.
Halafu madem wenyewe rahisi kuwapata kinoma. Omba namba tu mengine anajua mwenyewe. Na wengine ukiomba namba na usipomtafuta anakasirika saana. Wako wengi sana halafu hawana uhakika wa mapenzi. ‘Kozi’ kitaa masela wa sasa hawana ‘skilizi’.
Madogo wanajua ‘kukomenti’ mitusi mitandaoni. Lakini hayo matusi hawawezi kufanya kwa vitendo. Sisi zamani kupata hizo totozi ilikuwa mtihani sana, ilibidi tutumie akili nyingi sana kupata. Tulikuwa mafundi wa kushawishi na mbwembwe za uongo.
Hivi sasa kila sehemu kuna totoz za maana. Zamani madenti wa chuo mpaka uende Mlimani pale. Hivi sasa vyuo kibao kuanzia cha Mlimani, IFM, CBE, Tumaini hata vyuo vya ‘hoteli menejimenti’ pia kuna utajiri wa kina Eva na Delila. Na wote wako ‘singo’.
Acha ubwege. Miaka ya sasa hivi kile dem yupo ‘singo’. Ni wewe tu unaangalia jinsi ya kumpanga. Ni kwamba hapa Daslama hakuna ‘waifu’ wa mtu, omba namba tu. Wengi wapo kwenye ndoa kama fasheni au kuzuga watu. Maisha ya ‘usingo’ matamu zaidi kuliko ya ndoani.
Ukiishi kwenye ndoa hapa mjini huna tofauti na Tundu Lissu. Na wewe unakuwa mfungwa nje ya gereza. Na hili weka kichwani na ulifanyie kazi usibishe bishe tu kama bwege. Ndoa kwa mjini ni utumwa mtambuka ni sawa na kukosa demokrasia ya kweli ya akilini.
Zamani pisi zilisumbua kukubali zilipotongozwa. Na zilitusumbua sana kukubali siki ya ‘kideti’ tena zilisumbua sana kuingia getoni. Na zaidi zilitutesa sana kupanda au kukaa kitandani. Kimsingi pisi kukubali kubaki kama ilivozaliwa lilikuwa zoezi gumu kuliko lile la Tume ya Jaji Chande.
Na zaidi hata baada ya zoezi lote kukamilika bado alikasirika sana. Ukitaka kumuaga hataki umguse na hataki usemeshe. Anaondoka kanuna balaa utadhani alitekwa. Zamani mambo haya yalifanywa kibabe au kwa akili kubwa zaidi kuliko akili za Nyerere. Nomaa.
Kwenye balehe zetu miaka ya 90 mwishoni. Maeneo yetu yalikuwa ni ‘Slipwei’, Jumapili kuuza sura. Haikuwa lazima tuwe na totoz au tupate totoz. Kuuona uumbaji wa mola kwa viumbe uzao wa kike, kwetu ilikuwa faraja na maisha yalikuwa saaafi.
Nyakati zile ‘slipwei’ walijazana watoto wa kishua. Masela kutoka uswazi tulienda kutalii zaidi ya kutenda. Ubishi wa kutaka nawe uwe sehemu ya wakazi wa Dar na bata zake. Ndo uliotupeleka maeneo hayo ili tusimulie wana kitaa.
Lakini ukweli ni kwamba siyo kwa nguo tu, hata ngozi zetu na zao zilitofautiana. Kwa nyakati zile, ngozi ya mtoto mboga saba ungeiona lwa macho ya nyama. Yes! Kulikuwa na tofauti kubwa, na mavazi ndo balaa zaidi sasa.
Sisi watoto wa uswazi ‘shoping’ zetu ilkuwa ni mtaa wa Congo, Pemba, Tandamti, Mapipa kama siyo Manzese. Wa kishua wao waliletewa pamba na ndugu zao jamaa na marafiki. Tena ‘streiti’ kutoka unyamwezini kwenyewe.
Ukijichanganya sehemu lazima uone tofauti. Kuna ya pamba za kuletwa kwa begi na ndege toka Ulaya. Na pamba za kuletewa na balo kwa meli kutoka Ulaya. Kwa sababu zile za melini ni masalia ya nguo. Hayo ndo yalikuwa ndo maisha yetu.
Na uchakavu wa pamba zetu, bado tuling’oa pisi za kishua. Tulitegemea zaidi kupiga ‘fiksi’ na mbwembwe. Kitambo hicho sisi madingi ‘taim’ hiyo masela bado, tulikuwa na utajiri mkubwa wa maneno mbele ya viumbe wa kike. Unamuimbisha mtoto hadi analia.
Kuna pisi iliimbishwa na mchizi wangu. Wakati tunasoma Jiteute (Jitegemee), hadi dem ‘akafenti’. Tukaanza kumwagia maji huku tunampepea ndo akazinduka na kuomba maji. Wakati tuna balehe silaha kuu ilikuwa maneno. Piga kamba saana hai mtoto anaitikia kwa kichwa.
Achana na ‘slipwei’ kuna mitaa ya Posta pia. Huko tulikamata pisi ziizoagizwa barua, kununua kadi au pale Avalon kwenye sinema. Au kuna zile manzi zilipitapita ile mitaa ya ‘tauni’ na bahasha za kaki zikifukuzia ajira. Tulizirukia kinoma na hatukuwa na pesa au simu za mkononi.
Kwa sasa watu wako ‘bize’ sana kudiem’ madem. Hawana muda wa kufukuziana ‘marodini’ kama daladala. Shida ni moja tu, leo ni rahisi sana kupata madem, lakini ngumu sana kulipata penzi kweli kweli. Wanakutana kirahisi sana na kuachana kirahisi sana na ‘kuzagamuana’ kirahisi sana.
Leo Wema anamlilia Manunu. Kwa sababu alikuwa faraja yake. Watu wana upweke sana dunia ya leo. Na pia usishangae Kajala kurudiana na Konde Boy ‘deile’. Ni kwamba kupata ‘lavu’ ya kweli dunia ya sasa ni ngumu kinoma. Ndo maana kile dem yupo singo, na kila msela anapiga mingo.