#HABARI: Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Ole Millya, ametoa wito kwa jamii ya kifugaji kulinda rasilimali ardhi na kuepuka uuzaji holela ambao unaweza kuathiri mustakabali wa maisha yao.
Akizungumza mkoani Manyara, Ole Millya amesisitiza kuwa ardhi ni mali muhimu kwa wafugaji na inapaswa kutumiwa kwa tija ili kukuza uchumi wa familia badala ya kuifanya kuwa bidhaa ya kuuzwa.
Mhe. Ole Millya, ambaye pia ni Mbunge wa Simanjiro, ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi yaliyofanyika katika Kata ya Ruvu Remit.
Amesema kuwa wazazi na walezi wana jukumu la kuhakikisha ardhi inatunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo, huku akihimiza jamii hiyo kuweka mikakati thabiti ya kulinda maeneo yao ya malisho dhidi ya uvamizi au migogoro ya matumizi ya ardhi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)