
Tehran imejibu siku ya Jumapili pendekezo la Marekani, lililotolewa kupitia Pakistan, la kukomesha vita, licha ya makubaliano yausitihaji mapigano ambayo hayajazuia makabiliano yanayoendelea. Lakini jibu la Tehran halikupendeza Washington, ambayo imesema siku yaJumapili. Donald Trump ameandika kwenye jukwaa lake la Truth Social, kwamba jibu la Iran “halikubaliki kabisa.”
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Marekani hakutoa maelezo kuhusu maudhui ya jibu la Iran, anabainisha mwandishi wetu huko Atlanta, Edward Maille. Lakini kulingana na taarifa kutoka Gazeti la Wall Street Journal, Iran ilipendekeza kukomesha mgogoro huo na kufunguliwa taratibu kwa Mlango Bahari wa Hormuz, kwa sharti kwamba kizuizi cha Marekani cha meli za Iran kiondolewe. Pendekezo hili halikushughulikia madai ya Washington ya ahadi kuhusu akiba ya uranium iliyorutubishwa.
Iran ilipendekeza kwamba suala la nyuklia lijadiliwe ndani ya siku 30 zijazo. Lakini shirika la habari la Iran la Tasnim lilinukuu chanzo kilichodai kwamba ripoti ya Gazeti la Wall Street Journal kuhusu mapendekezo ya nyuklia ilikuwa ya uwongo.
Kwa hivyo ni vigumu kusema haswa ni wapi mazungumzo hayo yamekwama. Lakini katika mahojiano yaliyorushwa Jumapili kwenye kipindi cha CBS cha 60 Minutes, waziri mkuu wa Israel alisema kwamba vita havijaisha, na haivtaisha kutokana na Iran inamiliki uranium iliyorutubishwa kwa kiwango kikubwa na mitambo ya kurutubisha.
Iran ilijibu pendekezo la Marekani la kukomesha mgogoro siku ya Jumapili kupitia mpatanishi wa Pakistan. Hapo awali, Tehran ilitishia kulenga maeneo ya Washington katika Mashariki ya Kati ikiwa meli zake za kijeshi zitashambuliwa, baada ya mashambulizi ya Marekani dhidi ya meli zake mbili za mafuta.