Washington, moja ya wapatanishi katika mgogoro huu wa kikanda, inazisihi pande zote katika mgogoro huo kuweka kipaumbele mazungumzo, huku hali ya usalama ikiendelea kuzorota wiki hii katika maeneo kadhaa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, licha ya mazungumzo ya hivi karibuni huko Montreux, Uswisi, kati ya Kinshasa na wasi wa AFC/M23, yaliosimamiwa na Serikali ya Qatar.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo unatoka kwa Ofisi ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Marekani inalaani “shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya Mushaki” huko Kivu Kaskazini, pamoja na “mauaji” karibu na Uvira huko Kivu Kusini, mashariki mwa DRC, umesema ujumbe huo.

Washington haikutoa maelezo zaidi na haikunyooshea lawama upande wowote, lakini imetoa wito kwa “pande zote kujizuia,” kujitolea kutekeleza usitishaji mapigano, na kuweka kipaumbele mazungumzo.

Mapema, siku ya Ijumaa, Mei 8, waasi wa AFC-M23 waliishutumu jeshi la Kongo kwa kufanya shambulio baya la ndege zisizo na rubani huko Mushaki, mji ulio chini ya udhibiti wao, yapata kilomita 40 magharibi mwa Goma. Mashahidi waliripoti milipuko miwili mikubwa na hofu kubwa karibu na soko kubwa la Mushaki, ambalo huwa na watu wengi siku ya Ijumaa.

Waasi walitaja idadi kubwa ya vifo, ambayo hakuna chanzo huru kilichoweza kuthibitisha. Kinshasa, kwa upande wake, haijazungumza chochote kuhusu shambulio hilo

MONUSCO, kwa upande wake, imesema kuwa ina “wasiwasi mkubwa” na taarifa hii na imelaani “wimbi jipya la mashambulizi mabaya” yanayowalenga raia, ambayo yamesababisha makumi ya waathiriwa katika siku za hivi karibuni katika mikoa mitatu ya mashariki mwa DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *