
LICHA ya Kocha wa Mashujaa FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kuiongoza timu hiyo katika mechi nane za Ligi Kuu Bara bila ya kupoteza, amesema moja ya jukumu kubwa analofanyia kazi kwa sasa ni kutengeneza safu bora na kali ya ushambuliaji.
Akizungumza na Mwanaspoti, Julio amesema timu hiyo haina balansi nzuri katika eneo la kushambulia, ingawa kuna mwenendo mzuri wa safu ya kujilinda, hivyo kazi kubwa anayopambana nayo ni kuongeza kasi ya upatikanaji wa mabao kikosini humo.
“Ni jambo nzuri kama tunafunga mabao machache lakini tunaweza kuzuia wapinzani wetu wasifunge, ushindani wa nafasi kwa sasa ni mkubwa, hivyo ni lazima tuhakikishe maeneo yote tunaboresha ila mwishoni tupate kilichobora,” amesema Julio.
Julio aliyejiunga na kikosi hicho Februari 12, 2026, ameiongoza Mashujaa katika mechi nane za Ligi Kuu hadi sasa, kati ya hizo ameshinda mbili na kutoka sare sita, huku timu hiyo ikifunga mabao sita na kuruhusu matatu.
kocha huyo aliyewahi kuzifundisha Namungo FC na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ akiwa kocha msaidizi, amejiunga na Mashujaa akichukua nafasi ya Salum Mayanga anayeifundisha kwa sasa Mbeya City, aliyeondoka kikosini Februari 3, 2026.
Mayanga aliondoka Mashujaa ikiwa ni muda mfupi tangu timu hiyo ichapwe bao 1-0, dhidi ya KMC FC, huku kwa msimu wa 2025-2026, akiiongoza katika mechi 12 za Ligi Kuu, ambapo kati ya hizo alishinda tatu tu, akitoka sare nne na kupoteza tano.
Baada ya kuondoka Mayanga, timu hiyo ikaongozwa na Kocha Msaidizi, Charles Fred katika mechi mbili za Ligi Kuu, akianza na suluhu (0-0), dhidi ya Tanzania Prisons,