
Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso imemwita Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo, kukataa azimio lililopitishwa na wabunge wa Umoja huo kulaani uminywaji wa haki ya kujieleza na haki za msingi nchini humo tangu jeshi lilipoanza kutawala mwaka 2022.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wazriri wa Mambo ya nje wa Burkina Faso Jean-Marie Traoré Karamoko, amesema wamemlalamikia Balozi huyo wa EU Philippe Bronchain, na kukataa madai yaliyotolewa dhidi ya utawala wa kijeshi.
Burkina Faso inasema madai kuwa hakuna uhuru wa kujieleza, wakosoaji wa utawala wa kijeshi wanakamatwa na kuteswa ni uongo.
Aidha, Wizara hiyo inasema madai kuwa raia wanaotuhumiwa kushirikiana na makundi yenye silaha wanakamatwa, kuteswa na kuuawa sio za kweli, huku ikijitetea kuwa inaendelea kupambana na wanajihadi Pamoja na nchi jirani za Mali na Niger.
Azimio hili limekuja baada ya kuvunjwa kwa mashirika yote ya kiraia nchini Burkina Faso, ambayo pia imeishtumu utawala wa kijeshi kwa kuminya pia uhuru wa vyombo vya Habari.