
Nchini Mali, kukamatwa kwa washukiwa kuliendelea baada ya mashambulizi ya Aprili 25 kwenye miji na vijiji kadhaa. Mwendesha mashtaka wa umma katika mahakama ya kijeshi ya Bamako alitangaza kwamba uchunguzi umefunguliwa na kwamba wanajeshi na raia walihusika.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangu kufunguliwa kwa uchunguzi wa mahakama kuhusu mashambulizi ya Aprili 25, angalau askari na raia 19 wa Mali wamekamatwa.
Mountaga Tall amabye ni mwanasheria na mwanasiasa ambaye alitekwa nyara mapema Mei huko Bamako na watu waliojifunika nyuso zao na waliokuwa na silaha, anazuiliwa katika makao makuu ya huduma za kijasusi za Mali.
Yeye ni mmoja wa wanaoshukiwa kupanga shughuli hizo japo ndugu zake, wamekanusha madai hayo.
Aidha mwanajeshi wa zamani alidai katika video kwamba Mountaga Tall alikuwa mtu muhimu katika kuandaa mashambulizi.
Chama cha Wanasheria wa Mali kinataka kuachiliwa kwa Tall mara moja.