HUENDA Tanzania ikaandika historia ya kuwa na wachezaji wawili, baada ya mshambuliaji kinda Juma Sagwe kuelezwa anafanya majaribio kwenye kikosi cha Goztepe.

Ikumbukwe hapo awali Mbongo mwingine, Novatus Miroshi anayekipiga kwenye kikosi hicho huu ukiwa msimu wake wa pili akiwa ndiye kiungo tegemeo kwenye timu hiyo.

Kama Sagwe atafaulu majaribio hayo inaweza kuwa hatua moja ya kumfungulia milango ya soka la kulipwa Ulaya .

KIN 01

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Göztepe S.K. imekuwa ikivutiwa na vipaji kutoka Tanzania baada ya kumwona Miroshi akionyesha kiwango bora katika kikosi hicho, hali iliyofungua macho ya klabu hiyo kuangalia zaidi wachezaji kutoka Tanzania.

Sagwe kwa Tanzania ameitumikia KMC FC, hatua iliyompa msingi wa kujiamini na kupata uzoefu katika ligi ya ushindani.

Safari ya kinda huyo inaonekana kuwa ya kasi, kwani kutoka kucheza ligi ya Tanzania sasa amepewa nafasi ya kujaribu bahati yake katika moja ya ligi zinazoheshimika zaidi, jambo linaloashiria maendeleo ya vipaji vya Tanzania.

KIN 02

Taarifa zinaeleza makocha wa Göztepe S.K. wamekuwa wakifuatilia kwa karibu uwezo wake wa kumalizia mashambulizi, kasi yake pamoja na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali za ushambuliaji.

Mwita ni zao la programu ya kuibua vipaji ya Brazuka Sports Promotion Ltd, amekuwa miongoni mwa vijana waliopitia mchakato wa maendeleo ya soka baada ya kushiriki mashindano yaliyofanyika mikoa nane ya Tanzania bara na visiwani mwaka 2023, yakihusisha zaidi ya vijana 200.

Mkurugunzi wa Brazuka FC, Eric Mchatta amesema;

“Tunatamani mafunzo wanayopata vijana yawasaidie hadi nje waendelezwe vizuri na kusaidiwa, hilo ndio lengo letu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *