
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza leo Jumatatu, Mei 11, uwekezaji wa euro Bilioni 23 kwa Afrika, ikiwa ni pamoja na euro Bilioni 14 katika uwekezaji wa kibinafsi na wa umma wa Ufaransa pekee, wakati akifunga jukwaa la biashara la mkutano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na Afrika, Africa Forward, jijini Nairobi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Euro Bilioni 14 inajumuisha uwekezaji kutoka kwa wadau binafsi wa Ufaransa (makampuni, misingi, na fedha za uwekezaji) na miradi inayotengenezwa na mashirika ya misaada ya maendeleo ya Ufaransa (AFD, Proparco, na DG Trésor), kulingana na Ikulu ya Élysée. Euro Bilioni 9 zilizobaki zinatoka kwa wawekezaji wa Afrika.
Uwekezaji huu “utaunda zaidi ya ajira 250,000 za moja kwa moja nchini Ufaransa na Afrika,” ametangaza Emmanuel Macron, akisifu “matokeo halisi” ya mkutano huo ambao unafanyika Jumatatu na Jumanne katika mji mkuu wa Kenya. Kulingana rai Emmanuel Macron, hii inawakilisha utekelezaji wa “mabadiliko ya mantiki” anayotetea kwa uhusiano kati ya Ufaransa na Afrika. Kiasi hiki kinajumuisha aina zote za uwekezaji (moja kwa moja, usawa, ushirikiano) na vyombo vyote vya kifedha (hisa, mikopo, dhamana, ruzuku).
Emmanuel Macron atetea uwekezaji badala ya misaada ya umma
Afrika “inahitaji uwekezaji” badala ya misaada ya umma, ambayo Ulaya haiwezi tena kutoa kwa wingi hata hivyo, amesema Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo Jumatatu, siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa Ufaransa na Afrika jijini Nairobi.
Miongoni mwa sekta kuu zinazonufaika ni mpito wa nishati (euro Bilioni 4.3), teknolojia ya kidijitali na akili bandia (euro Bilioni 3.76), “uchumi wa bluu” (euro Bilioni 3.3 bilioni) na kilimo (euro bilioni 1), kulingana na Ikulu ya Élysée. Hata hivyo, uwekezaji wa euro Milioni 942 umetengwa kwa ajili ya sekta ya afya, euro Milioni 300 kwa ajili ya viwanda, na euro Milioni 250 kwa ajili ya sekta ya benki na fedha.