Rais wa DRC Félix Tshisekedi yuko Kampala leo kwa sherehe mbili tofauti: kumalizika kwa kikao cha 9 cha Kamati ya Pamoja ya Kudumu ya DRC-Uganda na, Mei 12, kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni. Ziara hii inasisitiza umuhimu ambao Kinshasa inaweka katika uhusiano huu: Uganda, ambayo ni mshirika wa kijeshi mashariki mwa Kongo, pia imekuwa mshirika mkuu wa kibiashara wa DRC. Hata hivyo, muungano huu una changamoto zake.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu wa uhusiano kati ya Kinshasa na Kampala si mpya. Umekuwa ukijengwa hatua kwa hatua tangu mwezi Novemba 2019, kupitia mfululizo wa mazungumzo ya ngazi ya juu. Mnamo mwezi Mei 2015, Vital Kamerhe, ambaye wakati huo alikuwa Spika wa Bunge la Kongo, alifanya ziara mjini Entebbe na ujumbe ulioelezewa kama maalum kutoka kwa Rais Félix Tshisekedi kwa mwenzake, Yoweri Museveni. Mwezi mmoja baadaye, majeshi ya DRC na Uganda yalitia saini mkataba huko Kinshasa ili kuendelea na Operesheni ya pamoja ya Shujaa dhidi ya wapiganaji wa ADF, wenye asili ya Uganda wanaohusishwa na Dola la Kiislamu, wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.

Leo, nchi hizo mbili zinataka kwenda mbali zaidi. DRC sasa ndiyo kitovu kikuu cha mauzo ya nje ya Uganda, ikiwa na ongezeko la 29% katika miaka miwili iliyopita na zaidi ya dola milioni 962 zilipokelewa mwaka wa 2024-2025. Lengo lililotajwa ni kuzidi kizingiti cha bilioni moja kiisha. Baarabara tatu zinajengwa ili kuwezesha uhusiano huu, ikiwa ni pamoja na barabara ya Mpondwe-Kasindi-Beni, inayofadhiliwa kwa pamoja na nchi hizo mbili. Hati sita za makubaliano zitasainiwa leo katika sekta mbalimbali kama vile biashara, uchukuzi, mawasiliano ya simu, na utawala.

Kauli za kushangaza

Lakini muungano huu haukosi mvutano wake. Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais Museveni na Mkuu wa majeshi wa  Uganda, amewatishia hadharani Wazalendo, wanamgambo wanaoshirikiana na vikosi vya Kongo, na kudai kuondoka kwa gavana wa kijeshi wa Ituri, Jenerali Johnny Luboya, mkoa ulioko kaskazini mashariki mwa DRC unaopakana na Uganda. Matamshi haya ya upande mmoja yalisababisha mvtano na Kinshasa.

Uwepo wa Tshisekedi katika sherehe ya kuapishwa kwa Museveni kesho unazungumzia hali ya uhusiano huu. Wakati Washington inajaribu kuzileta pamoja DRC na Rwanda kuhusu madini ya kimkakati, Kinshasa iko makini kutoitenga Uganda, jirani mwenye ushawishi na mdau muhimu wa kijeshi mashariki mwa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *