Dar es Salaam. Sekta ya michezo ya kubahatisha nchini Tanzania inaendelea kushuhudia ongezeko la ushindani mkali, huku kampuni mbalimbali zikiweka mkazo zaidi kwenye promosheni, bonasi na kampeni za zawadi kama njia ya kuwavutia na kuwabakiza wateja katika soko linalokua kwa kasi.

Mwelekeo huo umejidhihirisha kupitia kampeni ya ‘Upendo Unalipa na Jet X’ iliyoendeshwa na kampuni ya WasafiBet, ambayo imehitimishwa wiki hii kwa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki wa mchezo wa kasino wa Jet X.

Katika hitimisho hilo, mkazi wa Tunduru mkoani Ruvuma, Ally Ismail, amejinyakulia friji mpya ya milango miwili ikiwa ni zawadi kuu ya kampeni hiyo, ambayo imekuwa ikivutia washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Washindi wengine ni pamoja na Silvesta wa Mwanza aliyepata friji katika wiki ya kwanza ya kampeni, pamoja na Thadei Mtega na Agness Temba waliopata vocha za manunuzi zenye thamani ya Sh500,000 kila mmoja.

Akizungumzia kampeni hiyo wakati wa kukabidhi zawadi, Meneja Masoko wa Wasafibet, Selemani Mrisho, amesema promosheni hizo ni sehemu ya mkakati wa kampuni kuimarisha ushiriki wa wateja na kuongeza hamasa katika michezo ya mtandaoni.

“Promosheni hii ilikuwa inalenga kuwazawadia wateja wanaoshiriki mchezo wa Jet X. Tumepata mwitikio mkubwa kutoka maeneo mbalimbali nchini, na licha ya kampeni hii kuhitimishwa, kampuni itaendelea kuendesha promosheni na bonasi nyingine kwa wateja,” amesema.

Amesema kampeni ya ‘Upendo Unalipa na Jet X’ imepokelewa vyema na wateja kutoka maeneo mbalimbali nchini, akibainisha kuwa kampuni hiyo itaendelea kuendesha promosheni na bonasi nyingine katika kuhakikisha inaboresha uzoefu wa wateja wake.

Wakati huohuo, wadau wa sekta hiyo wanasema ukuaji wa matumizi ya simu janja na huduma za fedha kwa njia ya simu umekuwa chachu ya kupanuka kwa michezo ya kubahatisha mtandaoni, hali inayoongeza ushindani kati ya kampuni zinazotoa huduma hizo.

Hata hivyo, ongezeko hilo linaendelea kuibua mjadala kuhusu umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo pamoja na kuhamasisha uwajibikaji kwa watumiaji, hususan vijana ambao ndio watumiaji wakubwa wa majukwaa ya kidijitali ya michezo ya kubahatisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *