
Dodoma. King’ora cha kuonyesha hali ya hatari kimeleta taharuki ndani ya Bunge na kufanya baadhi watoke nje.
Hata hivyo, sekunde chache baadae Mwenyekiti wa Bunge, Deo Mwanyika amewatoa hofu wabunge kwamba ilikuwa hali ya kawaida.
Kengere inayoashiria kuna hatari ilitoa mlio wa king’ora wakati Mbunge wa Dimani, Nabil Ahmed Abdallah alipokuwa akichangia kwenye Hotuba ya Wizara ya Uchukuzi.
Hii si mara ya kwanza kwa king’ora kutoa mlio huo kwani mara ya kwanza ilikuwa Februari 5, 2019 ambapo Wabunge walitimua mbio wakiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage.
Mara ya pili hali hiyo ilitokea tena Juni 23, 2023 lakini aliyekuwa Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson aliwatuliza wabunge kwamba ilikuwa hali ya kawaida na kuwataka kuwa watulivu.