Changamoto ya ukosefu wa mitaji imeendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa wafungwa wanaotoka gerezani kuanza maisha mapya, licha ya baadhi yao kupata mafunzo ya ujuzi mbalimbali wakiwa vifungoni.
Kutokana na hali hiyo, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameagiza Jeshi la Magereza kuanzisha mfuko maalum utakaowasaidia wafungwa waliomaliza vifungo vyao kujikwamua kiuchumi na kuanzisha shughuli za kujipatia kipato.
Kauli hiyo imeibua matumaini mapya kwa wafungwa wanaorejea katika jamii, huku hatua hiyo ikitarajiwa kusaidia kupunguza changamoto za kiuchumi na kuwapa fursa ya kuanza maisha mapya kwa kujitegemea.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)