Wizara ya Uchukuzi imewasilisha bajeti yake bungeni huku wabunge wakihimiza matumizi makubwa ya Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani, ili kusaidia kupunguza msongamano wa magari, uharibifu wa miundombinu na foleni za barabarani katika jiji la Dar es Salaam zinazochangiwa na ongezeko la bandari kavu ndani ya jiji hilo.

Wabunge hao wameeleza kuwa matumizi bora ya Bandari ya Kwala yanaweza kusaidia kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kupunguza mzigo mkubwa wa malori yanayoingia katikati ya jiji.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *