
Rais wa China, Xi Jinping ametoa wito kwa nchi yake na Marekani kushirikiana kama washirika badala ya kuwa wapinzani, akisisitiza haja ya utulivu katika uhusiano wa mataifa hayo mawili yenye ushawishi mkubwa duniani.
Taarifa iliyotolewa na BBC inaeleza Xi ameeleza hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mazungumzo yake na Rais wa Marekani, Nonald Trump aliyepo nchini humo kwa ziara ya siku mbili, ambapo alibainisha kuwa dunia nzima inayafuatilia mazungumzo yao.
Aliongeza kuwa dunia imefika katika njia panda mpya, akihoji iwapo China na Marekani zinaweza kuepuka kile kinachoitwa ‘mtego wa Thucydides’ (nadharia ya siasa za kimataifa inayomaanisha kuwa vita au mzozo mkubwa unaweza kutokea pale dola kubwa iliyopo madarakani (dominant power) inapohisi kutishiwa na dola mpya inayoinuka (rising power). Ameshauri badala yake nchi hizo kuanzisha mfumo mpya wa mahusiano unaoweza kuleta utulivu wa kimataifa.
Xi amehoji pia iwapo mataifa hayo mawili yanaweza kushirikiana kukabiliana na changamoto za dunia na kujenga mustakabali bora wa mahusiano yao kwa masilahi ya watu wao na binadamu kwa ujumla.
Pia amewapongeza Marekani na Rais Donald Trump kwa kuadhimisha miaka 250 ya uhuru, akisema nchi hizo mbili zina masilahi mengi yanayofanana kuliko tofauti.
Amesisitiza kuwa mafanikio ya upande mmoja yanaweza kuwa fursa kwa mwingine, na kwamba uhusiano thabiti kati ya China na Marekani ni muhimu kwa utulivu wa dunia.
“China na Marekani zinanufaika na ushirikiano na hupoteza kupitia migogoro,” amesema, akihitimisha kwa wito wa mataifa hayo kuwa washirika na kusaidiana kufanikiwa katika enzi mpya ya mahusiano ya kimataifa.
Mapigano hayo yaliwahusisha wananchi na watu waliotajwa kuwa mabaunsa waliodaiwa kupelekwa na Ngololo ili kubomoa nyumba zilizojengwa eneo hilo, hali iliyosababisha vifo vya watu wanne, majeruhi na uharibifu wa mali.
Mei 12, maofisa kutoka Halmashauri walikwenda kufanya tathimini ya uharibifu katika eneo hilo na kuondoka huku wananchi walioathirika wakisema bado hawajui hatma yao.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John (Niki wa Pili) aliiambia Mwananchi kwamba Serikali ya wilaya ilijaribu kusuluhisha mgogoro wa ardhi uliokuwepo baada ya kutokea uvamizi ambapo wenye maeneo 121 waliridhia wavamizi wawalipe isipokuwa familia ya Ngololo.
Alisema kabla ya vurugu hizo kulikuwa na mchakato wa maridhiano kati ya wananchi waliokuwa wamejenga eneo hilo (wavamizi) na baadhi ya wamiliki halali, ambapo walikubaliana waliuziwa maeneo hayo kwa utapeli na kuwa tayari kuyalipia upya kwa gharama ya Sh3,000 hadi Sh3,500 kwa kila mita ya mraba.
“Familia ya Ngololo haikukubaliana na maridhiano hayo na badala yake ilitaka suala hilo liamuliwe mahakamani, hivyo mgogoro wa ardhi uliopo eneo hilo utamalizwa na mahakama, kuhusu vurugu zilizotokea tayari mtuhumiwa amekamatwa kwa uchunguzi zaidi,” alisema.
Familia 10 zilizopoteza makazi katika vurugu hizo na kupata hifadhi kwenye mapagale huku zikisaidiwa chakula kupitia michango ya wadau mbalimbali iliyokusanywa na uongozi wa Serikali ya Mtaa na majeruhi ambao walipelekwa hospitali ya mkoa ya Tumbi wakiendelea na matibabu.