Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga limejipanga kuimarisha ulinzi shirikishi katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo kufuatia kuongezeka kwa matukio ya kiuhalifu yanayoripotiwa katika baadhi ya maeneo.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Dadi Colimba amesema ni muhimu kwa viongozi pamoja na wananchi kushirikiana katika kuhakikisha amani na usalama vinaendelea kuimarika ndani ya Jiji la Tanga.

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Colimba amesema baadhi ya maeneo yamekuwa yakikumbwa na vitendo vya kihalifu hali inayohitaji nguvu ya pamoja kupitia mfumo wa ulinzi shirikishi.

Amesema kutokana na maazimio yaliyopitishwa na baraza hilo, serikali itaanza zoezi la usajili wa vituo vya waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, hatua inayolenga kudhibiti baadhi ya vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na watu wanaotumia usafiri huo na kusababisha uvunjifu wa amani.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Selebosi Mustafa amewataka watendaji wa halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi, uwajibikaji pamoja na kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili jiji hilo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *