Kuongezeka kwa talaka nchini kumeendelea kutajwa kuwa chanzo kikubwa cha kudhoofika kwa ustawi wa jamii, kupungua kwa nguvu kazi, na kuongezeka kwa shinikizo la huduma za kijamii kwa serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Isaya Mbenje, amesema hali hiyo pia inahatarisha mafanikio ya malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga familia imara na jamii yenye mshikamano.
Akifungua mafunzo ya wajumbe wa bodi za usuluhishi wa ndoa wilayani humo, Mbenje amesisitiza umuhimu wa kuimarisha taasisi ya ndoa na kuweka mikakati madhubuti ya kupunguza migogoro ya kifamilia.
Amesema talaka huongeza changamoto za kijamii na kuilazimu serikali kubuni sera zaidi za kusaidia familia zilizovunjika.
Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Zerafina Gotora, amezitaka bodi hizo kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kutunza siri za wanandoa, ili kurejesha amani na mshikamano katika jamii.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)