Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar imeanza maandalizi ya ushiriki wake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Julius Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa – Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Habiba Hassan Omar, wakati alipofanya ziara katika viwanja hivyo na kukagua banda la Zanzibar ambalo huonesha bidhaa mbalimbali kutoka visiwani humo.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *