Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Aristides Mbwasi amesema asilimia 70 ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unategemea mchango wa sekta binafsi, ikiwemo wafanyabiashara na wawekezaji, hivyo Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowezesha sekta hiyo kukua na kuchangia maendeleo ya uchumi.
Mbwasi alitoa kauli hiyo wakati wa kongamano la sheria za ushindani na wawekezaji Tanzania lililolenga kukuza biashara na uwekezaji nchini, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuimarisha mazingira bora ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi na kuongeza ushindani wa kibiashara.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)