Marekani. Rapa na mtayarishaji wa muziki wa Marekani, Khaled Mohamed Khaled maarufu Dj Khaled ameonyesha muonekano wake mpya ukimuonyesha amepungua uzito kwa kiasi kikubwa na kuzua gumzo mitandaoni.

Kwenye video aliyoichapisha kwenye mtandao wa Instagram mtayarishaji huyo  mwenye umri wa miaka 50, alionekana mwembamba zaidi katika video hiyo na kuzua mijadala mitandaoni.

Katika video hiyo, DJ Khaled alionekana akiwa amevaa mavazi ya buluu yaliyomuonyesha vizuri  mwonekano wake mpya, tofauti kabisa na jinsi alivyozoeleka kuonekana miaka ya nyuma akiwa mnene.

KHALEE 01

Baadhi ya mashabiki walitoa maoni kwenye mtandao wake wa kijamii wengine wakimpongeza kwa mabadiliko hayo na wengine walikuwa na mshangao wa kupungua ghafla kwa mkali huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Grammy.

Ikumbukwe mwaka 2026, DJ Khaled alitangaza  kuwa ameanza safari ya kuboresha afya yake kwa kupunguza uzito na kuongeza mazoezi ya kila siku. Alieleza kuwa anatembea kati ya hatua 10,000 hadi 15,000 kila siku, huku wakati mwingine akifikia hatua 20,000.

KHALEE 02

Aliongeza kuwa mchezo wa gofu umekuwa sehemu muhimu ya mafanikio yake. Kwa mujibu wake, gofu humsaidia kutembea umbali mrefu na kuchoma mafuta bila kuhisi uchovu mkubwa..

Katika ujumbe wake, DJ Khaled alisema lengo lake ni kuwa na afya bora ili awe baba na mume bora zaidi kwa familia yake. Alisisitiza kuwa mafanikio haya ni mwanzo tu wa safari yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *