Man City bingwa FA ikiichapa Chelsea fainaliMan City bingwa FA ikiichapa Chelsea fainali

London. Man City imetwaa ubingwa wa Kombe la FA baada ya leo Jumamosi, Mei 16, 2026 kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea katika fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Wembley, London.

Bao pekee lililoihakikishia taji Man City katika mechi hiyo limepachikwa na Antoine Semenyo katika dakika ya 72 akimalizia kwa ustadi kwa mguu wa kulia pasi ya Erling Haaland.

Hilo ni taji la pili kwa Man City kuchukua msimu huu baada ya kufanya hivyo kwa kutwaa taji la Calabao kwa kuichapa Arsenal kwa mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa Machi 22, mwaka huu.

Man City ina nafasi ya kumaliza msimu huu ikiwa na mataji matatu (treble) ikiwa pia itafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL).

Ushindi wa leo pia unamfanya Meneja wa Man City, Pep Guardiola awe ameiongoza timu hiyo kutwaa mataji 20 katika kipindi cha miaka 10 aliyoiongoza.

Kwa upande mwingine matokeo hayo yamezika rasmi ndoto za Chelsea kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwani haiwezi kumaliza katika nafasi tano za juu kwenye msimamo wa EPL.

Ni matokeo ambayo yameendeleza nuksi ya Chelsea katika mashindano ya Kombe la FA kwani ni fainali ya nne mfululizo kwa timu hiyo kupoteza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *