
Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta ameshinda tuzo ya Meneja Bora wa Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2025/2026.
Arteta ametangazwa jana Jumanne, Mei 26 katika hafla ya utoaji wa tuzo hiyo iliyofanyika London, England.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Arteta kushinda tuzo hiyo tangu alipoanza kuinoa Arsenal mwaka 2019.
Ushindi huo kwa Arteta umekuja siku chache baada ya kuiongoza Arsenal kutwaa taji la EPL ambalo ni la kwanza kwa timu hiyo tangu ilipofanya hivyo miaka 22 iliyopita.
Pia Arteta amekuwa meneja wa kwanza kupata ushindi wa tuzo ya Meneja Bora wa msimu kwenye EPL tangu Arsene Wenger alivyofanya hivyo msimu wa 2003/2004.
Pia amekuwa meneja wa kwanza kushinda tuzo hiyo akiwa meneja wa timu aliyowahi kuichezea.
Umekuwa msimu bora kwa Arsenal chini ya Arteta ambapo imetwaa ubingwa wa EPL baada ya kukusanya pointi 85.
Timu hiyo imeruhusu mabao 27 tu ambayo ni machache zaidi huku pia ikimaliza msimu ikiww haijaruhusu penalti wala kupata kadi nyekundu.
