Vijana wajasiriamali toka maeneo mbalimbali wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kifedha ili kuwawezesha kupata mitaji kwa ajili ya kukuza na kuendeleza biashara zao.
Mafunzo hayo yametolewa jijini Dodoma kupitia kikao cha maarifa kilichoandaliwa na Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Tanzania (CEOrt), kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania Foundation na Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania, TWCC, chini ya programu ya Think Equal Lead Smart.
Akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Miradi wa CEOrt, Hawa Urungu, amesema changamoto ya upatikanaji wa mitaji bado ni kubwa kwa vijana wengi licha ya kuwepo kwa mafunzo mbalimbali.
Washiriki wa mafunzo hayo wameelekezwa umuhimu wa nidhamu ya kifedha, utunzaji wa kumbukumbu za biashara, uwekaji wa akiba, matumizi ya mifumo ya kidijitali na uwekezaji wa faida.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa TWCC, Naima Nyange, amesema vijana wengi wanakumbana na changamoto za dhamana na historia ndogo ya kifedha.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)