Jenna, binti mfalme aliyegeukia kwenye muziki, ugizajiJenna, binti mfalme aliyegeukia kwenye muziki, ugizaji

Cambodia.  Akiwa mmoja wa watoto wa kifalme wanaofuatiliwa zaidi barani Asia. Princess Norodom Jenna ameendelea kuvutia wengi kupitia muziki, uigizaji na uwezo wake wa kuzungumza lugha mbalimbali. 

Norodom Jenna alizaliwa Machi 11, 2012 jijini Paris, Ufaransa. Ni binti kutoka familia ya kifalme ya Cambodia ambaye alimpata na mfanyabiashara raia wa Ufaransa. Pia Jenna ni kitukuu cha marehemu mfalme Norodom Sihanouk na ndugu wa karibu na mfalme wa sasa wa Cambodia, Norodom Sihamoni.

Aliishi jijini Paris kwa miaka mitatu tu kisha familia yake ikahamia Cambodia mwaka 2015. Ambapo alianza kuishi maisha ya kifalme, alipata elimu pamoja na mafunzo ya sanaa, Music Arts School iliyopo Phnom Penh.

Aidha moja ya vitu vilivyomtofautisha Jenna ni uwezo wake wa kuzungumza lugha tano ambazo ni Khmer, Kifaransa, Kiingereza, Kithai na Kichina. Uwezo ambao umemsaidia kuvuka mipaka ya Cambodia na kupata mashabiki kutoka mataifa mbalimbali ya Asia na Ulaya.

Wapo wengi wanaoamini kuwa ukizaliwa katika familia ya kifalme unatakiwa kuwa mbali na mitandao ya kijamii pamoja na mambo yanayoweza kuondoa hadhi ya kifalme. Lakini kwa Jenna imekuwa tofauti kwani kupitia akaunti zake za YouTube, TikTok na mitandao mingine, amekuwa akionesha kipaji chake kinachokubaliwa na watu kutoka mataifa mbalimbali.

Hata hivyo, alijitosa kwenye muziki mazima akianza kwa kuimba nyimbo za lugha mbalimbali pamoja na kufanya cover za nyimbo za K-Pop. Huku akiwakosha wengi kwa staili yake ya kucheza inayofanana na msanii Lisa kutoka kundi la BLACKPINK.

Baada ya hatua hiyo aliingia rasmi katika muziki akitoa ngoma kama ‘Falling’ na Truth or Game’, zilizoongeza umaarufu wake katika muziki ambapo kwasasa amepanga kuachia albumu yake ya kwanza aliyoipa jina la Mandarin.

Mbali na muziki, Jenna pia anatambulika kama mwigizaji, ambapo alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka sita huku kazi zake zikionekana katika televisheni ya taifa ya Cambodia.

Mwaka 2024, Jenna alifanikiwa kushinda tuzo ya Best Newcomer Actress katika tuzo za ‘Cambodia-Asia Film Festival’ kutokana na uigizaji wake kwenye filamu ya kutisha ya “The Night Curse of Reatrei,”. 

Kutokana na mvuto wake na ushawishi mkubwa kwa vijana, Jenna pia amekuwa balozi wa brand mbalimbali za kimataifa na zikiwemo Cellcard Telecommunications, Marie Regal, R&F Properties pamoja na OPPO. Pia amewahi kuwa balozi wa Cambodia Dance Sport Federation.

Mbali na sanaa, Jenna ameendelea kuheshimiwa kwa juhudi zake za kuutangaza utamaduni wa Cambodia kimataifa. Ameonekana kwenye majukwaa mbalimbali ya kimataifa akizungumza na kufanya maonesho ya kitamaduni, ikiwemo Beijing Cultural Forum, jambo lililomfanya kuonekana kama daraja linalounganisha utamaduni wa Asia na dunia.

Kutokana na mwonekano wake, uwezo wa kucheza, mvuto wake jukwaani na heshima yake mbele za watu zimekuwa zikiwafurahisha mashabiki wengi huku wengi wakimtaja kama mmoja wa watoto wa kifalme wenye ushawishi mkubwa zaidi barani Asia kwa sasa na ambao wanaheshimu kila mtu.

Mwezi Aprili 2026, Mfalme Norodom Sihamoni alimpa rasmi hadhi ya “Her Royal Highness” ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika kuitangaza sanaa, utamaduni na taswira ya Cambodia duniani kote.

Her Royal Highness ni cheo kinachotambulika kama ‘Mwanafalme mwenye hadhi ya juu ya kifalme’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *