Migogoro ya ardhi 5,573 yatatuliwaMigogoro ya ardhi 5,573 yatatuliwa

DODOMA; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Leonard Akwilapo, amesema hadi Mei 15, 2026, jumla ya migogoro ya ardhi 5,573 ilitatuliwa.

“Katika mwaka 2025/26, wizara ilipanga kushughulikia migogoro ya ardhi 3,000. Hadi tarehe 15 Mei 2026, jumla ya migogoro ya ardhi 5,573 imetatuliwa ambapo kati ya hiyo, migogoro 3,183 imetatuliwa kupitia Kliniki za Ardhi na 2,390 kupitia utaratibu wa kawaida wa kiutawala,” amesema Dk Akwilapo akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo Mei 28, 2026 na kuongeza:.

“Katika mwaka 2026/27, wizara imepanga kushughulikia migogoro 4,000 kiutawala. Natoa rai kwa viongozi, watumishi na wananchi kwa ujumla kuzingatia sheria za ardhi, kanuni na miongozo ili kuepuka kuanzisha migogoro mipya,” amesema Waziri Akwilapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *