Imeelezwa kuwa Hali ya utulivu wa nchi pamoja na Uongozi bora na imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ni kivutio cha wawekezaji kuja kwa wingi kuwekeza nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Komredi Kenani Kihongosi wakati alipotembelea Bustani ya Wanyama ya Serval Wildlife iliyopo Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro katika yake Wilayani humo ambapo amesema katika kipindi cha mwaka 2023/24 Idadi ya Watalii iliongezeka ambapo jumla ya watalii laki tisa na elfu 22 waliingia nchini kuja kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo mbuga za Wanyama.

Aidha Kihongosi amesema kupitia filamu ya The Royal Tour iliyofanywa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ilichangia kwa asilimia kubwa ukuaji wa sekta ya utalii nchini ikiwemo ongezeko kubwa la wageni walioingia nchini kuja kutalii.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *