Wafanyakazi mashariki mwa DR Congo wanajenga upya kituo cha matibabu ya Ebola ambacho kilichomwa moto na waandamanaji mapema mwezi huu, huku maafisa wa afya wakionya kwamba taarifa potofu zinawafanya familia kuwaficha ndugu zao walioambukizwa virusi vya Ebola.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Kongo imethibitisha zaidi ya wagonjwa 1,000 wanaoyoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola na vifo 220 tangu mlipuko huo utangazwe.

Umati wa watu wenye hasira ulichoma moto sehemu ya hospitali katikati ya mlipuko wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya familia na marafiki wa kijana anayeaminika kufariki kutokana na virusi hivyo kunyimwa ruhusa ya kuchukua mwili wake kwa mazishi.

Mwanasiasa mmoja wa akinukuliwa na BBCalisema baadhi ya ndugu wa marehemu huyo hawakuamini kuwepo kwa virusi hivyo, ambavyo hadi sasa vimewaua zaidi ya watu 130 mashariki mwa DRC. Katika machafuko yaliyofuata tukio hilo, polisi walifyatua risasi za onyo ili kutawanya umati.

Mwili wa mwathiriwa wa Ebola unaambukiza haraka, na mamlaka lazima zihakikishe mazishi salama ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza “mazishi salama na ya heshima” kwa waathiriwa wa Ebola, huku timu zilizofunzwa zikitumia vifaa vya kinga kushughulikia miili hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *