Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuhakikisha mradi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Kimataifa cha Moshi cha Ngangamfumuni unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi, kuongeza mapato ya Halmashauri na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kihongosi ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 28, ambapo amebainisha kuwa tayari Serikali imetoa zaidi ya Shilingi bilioni 19 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo baada ya mradi kusimama kwa muda kutokana na changamoto za kifedha.
Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Kihongosi amesema ameridhishwa na kiwango cha utekelezaji kilichofikiwa na kwamba ubora wa kazi unaonyesha thamani halisi ya fedha za umma zilizowekezwa.
Amesisitiza wananchi wa Moshi kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo kwani ni mali yao na kwamba ikiharibiwa hasara itakuwa kwa wananchi wenyewe pamoja na Serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe amesema mradi huo ulianza mwaka 2019 lakini ulisimama kutokana na changamoto za kibajeti kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita kuingilia kati na kutoa fedha za kuukamilisha.
Amesema hadi sasa zaidi ya Shilingi bilioni 12.7 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huo ambao umefikia hatua mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo kuu la abiria, maegesho ya magari, mifumo ya maji na umeme pamoja na maeneo ya biashara.
Mwajuma amesema mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 100 kwa wakati mmoja, magari madogo zaidi ya 1,000, maduka 26 ya biashara, vibanda vya tiketi 25, ofisi mbalimbali za huduma pamoja na kumbi za mapumziko kwa abiria.
Katika hatua nyingine, Kihongosi amepongeza Manispaa ya Moshi kwa utekelezaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa vijana, wanawake na watu
(Feed generated with FetchRSS)