Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Komredi Kenani kihongosi amehitimisha ziara yake katika mkoa wa Kilimanjaro kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Snow View Wilayani Hai mkoani humo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Akihutubia katika mkutano huo Kenan Kihongosi amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM Chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa chama hicho ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dr Samia Suluhu Hassan kimeleta maendeleo mengi na makubwa katika mkoa huo wa Kilimanjaro na kwamba chama hicho kitaendelea kufanya kazi ya kujenga nchi na kuwatumikia Watanzania kwa uaminifu mkubwa.

Pia katika mkutano huo Kihongosi aliwasihi wananchi wa Wilaya hiyo ya Hai kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kujiepusha na vitendo vya uchochezi vitakavyohatarisha amani ya nchi.
Katika ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuimarisha uhai wa chama ngazi ya mashina Komredi Kihongosi alikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika Wilaya za Siha, Moshi na Hai ambapo pia alikagua uimara na uhai wa chama mashinani pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Leo Katibu Mwenezi huyo anaanza ziara ya kichama ya siku tatu katika mkoa wa Manyara ambako nako atakagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, atatembelea mashina kwa ajili ya kuangalia uhai wa chama na atafanya mikutano ya hadhara kwa lengo la kuzungumza na wanachi na kusikiliza kero zao.

Wilaya atakazotembelea katika mkoa huo ni Hanang, Simanjiro na Babati.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *