Waumini wa Kanisa Katoliki mkoani Tabora wamehimizwa kutokata Tamaa katika maisha, bali waendelee kumtumikia Mungu na kulitumikia Taifa kwa ujumla huku wakisisitizwa umuhimu wa kuwa na moyo thabiti katika mapambano ya kutafuta maisha, bila kuangukia katika vitendo visivyofaa kama wizi, ujambazi na vitendo vinavyovuruga amani ya jamii sawa na kuishi kwa nidhamu, bidii na uadilifu ili kujenga jamii yenye maadili na ustawi bora.
Hayo yamesemwa na Mwadhama Askofu Mkuu wa jimbo kuu katoliki Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa wakati wa harambee ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa katoliki la Mtakatifu Bernadetha lililopo Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora,akisisitiza umuhimu wa waumini kuwa wavumilivu, wachapakazi na waadilifu katika kujenga maisha yao na kuchangia maendeleo ya Taifa na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali.
@deilahmomo
(Feed generated with FetchRSS)