Timu 34 zitashiriki katika mashindano ya kusaka vipaji vya soka ya Tulia Trust Uyole Cup ambayo yamezinduliwa leo mkoani Mbeya.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda amesema mashindano hayo yanapaswa kutumika vyema ili yaendelee kuwa daraja la mafanikio kwa vijana kisoka.
“Mpira wa miguu si burudani pekee, ni uchumi, ajira na fursa za maisha. Vijana wanapaswa kutumia mashindano haya kujitangaza na kufikia ndoto zao,” amesema Itunda.
Mratibu waTaasisi ya Tulia Trust ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo, Lugano
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda akizungumza na kufungua mashindano ya ligi ya Tulia Trust Uyole Cup 2026,msimu wa saba katika viwanja vya Mwawinji Bonde la Uyole.Picha na Hawa Mathias
Mwangosi, amesema tangu yalipoanzishwa, yamekuwa na tija kwa vijana.
“Haya ni matokeo ya dhamira ya dhati ya Dk Tulia ya kuwajengea vijana mazingira ya kukuza vipaji vyao, lakini kuwafungulia milango ya ajira na maendeleo ya kiuchumi,” amesema Mwangosi.
Kwa mujibu wa waandaaji, bingwa wa msimu huu atazawadiwa Sh10 milioni, mshindi wa pili Sh5 milioni na mshindi wa tatu Sh3 milioni.
Pia, zawadi ya Sh100,000 itatolewa kwa mfungaji bora, golikipa bora, mwamuzi bora, mchezaji bora na kocha bora, huku kikundi bora cha uhamasishaji kikijishindia Sh200,000.