
Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kesho anatarajia kuzindua mradi wa upimaji ardhi kidijitali wenye thamani ya Euro 37 milioni (Sh111.187 bilioni).
Mradi huo unaojulikana kama Land Administration and Regulatory Information System (Laris), utanziduliwa kesho Julai 27, 2026 kwa kutumia ndege maalumu itakayokusanya taarifa za ardhi Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mradi huo leo Julai 26, 2026 katika uwanja huo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Katibu Mtendaji kamisheni ya ardhi, Mussa Kombo Bakari amesema mradi huo wa miaka miwili, wanatarajia kupima vipande vya ardhi 25,000.
“Uzinduzi hasa utafanywa kwa tukio la ishara ya kuzindua ndege rasmi itakayotumika katika kuchukua picha za anga na hasa taarifa za ardhi ambazo zitaweza kuibadilisha sura ya ardhi hapa Zanzibar kutoka katika analojia kwenda katika sura ya kidijitali.
Amesema ndege hiyo kutoka Ufaransa, tayari imeshawasili na itaturuka miezi mitatu, katika kipindi cha jumla ya saa 34 juu ya anga.
Katibu huyo mtendaji, amesema baada ya kukamilika kwa kazi hiyo wanaamini itaboresha namna ya upatikanaji wa taarifa tofauti na ilivyo sasa, ambapo hukumbwa na dosari kutokana na kutumia teknolojia ambayo imepitwa na wakati.
Kiasi hicho cha fedha ni mkopo uliochukuliwa na Serikali kutoka Benki ya BPI ya Ufaransa asilimia 85 na asilimia 15 kutika Benki ya CRDB.
Kwa mujibu wa upimaji huu mwingine utakaoendelea baadaye itakuwa kuna mfumo rasmi ambao taarifa hizo zitaingizwa.
Kwa muda mrefu sekta ya ardhi ina idara mbalimbali kila moja imekuwa ikifanya kazi kivyake hivyo mfumo huo utaziunganisha idara zote na kurahisisha kuona taarifa za idara zote kwa wakati mmoja.
Mnemo Issa Haji, mkazi wa Nungwi amesema huenda mpango huo ukasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwani imekuwa ikiongezeka kila kukicha kutokana na sehemu kubwa ya ardhi kutopimwa