Rais wa Rwanda Paul Kagame, akiwa ziarani nchini Ufaransa, na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wamezindua mnara wa pande mbili kwenye kingo za Mto Seine jijini Paris Jumanne alasiri, Juni 2, kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi, ambayo yalisababisha vifo vya watu milioni moja. Mnara huo, ulioundwa kama mahali pa ukumbusho, uko karibu na Quai d’Orsay.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jeanne Uwimbabazi, mmoja wa manusura wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda, ambaye alikuwa Paris mnamo Juni 2, alitoa simulizi la kugusa moyo la siku alizopoteza familia yake, marafiki, na majirani. Alizungumzia ukumbusho uliozinduliwa siku hiyo katika mji mkuu wa Ufaransa kama “faraja ,” aina ya “malipo ya kiishara.”

“Kutekeleza majukumu ya kihistoria ya mtu kunahitaji ujasiri wa kweli, kwani huchochea upinzani mkali kutoka kwa wale wanaopaswa kujibu kwa matendo yao. Inahitaji ubinadamu mkubwa ili kutimiza hili hadi mwisho. Mheshimiwa Rais Macron, napenda kukupongeza kwa yote mawili: ujasiri wako na ubinadamu wako.”

“Ufaransa haikuwa nchi pekee iliyoshindwa. Nchi zingine nyingi pia zilishindwa, lakini hakuna hata moja iliyofikia (…) katika kuthibitisha ukweli na kutambua sehemu yake ya jukumu katika mauaji hayo ya kutisha,” aliongeza Paul Kagame.

Mkuu wa nchi ya Rwanda alisifu hatua yenye hatari kubwa iliyochukuliwa na rais wa Ufaransa mnamo 2021 alipokiri jukumu la Ufaransa, akisema kwamba “ingeweza kusitisha mauaji ya kimbari lakini ilikosa utashi.” Paul Kagame hajasahau maneno haya. “Ninaona matamshi haya kuwa ya thamani zaidi kuliko kuomba msamaha, yaani ukweli,” alibainisha mnamo Juni 2. Kwa upande wake Emmanuel Macron alimshukuru Paul Kagame kwa dhati kwa “kukubali utambuzi huu” na kusifu “uhusiano uasio wa kawaida” ambao “umeibuka” kati ya Ufaransa na Rwanda katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Rais wa Ufaransa anaona mnara uliozinduliwa Paris kama “kilele” cha mchakato wa ukumbusho kati ya nchi hizo mbili. “Sasa unaashiria mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda katikati ya mji mkuu wetu na historia yetu. Ni kilele cha kazi ndefu na ya uvumilivu ya ukweli ambayo tumekumbatia kwa pamoja na ambayo inategemea miongo kadhaa ya ushuhuda, maandishi, utafiti, na uhamasishaji usiyotetereka,” alisema Emmanuel Macron.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *