
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amependekeza mkutano wa moja kwa moja na mwenzake wa Urusi katika barua kwa Vladimir Putin iliyochapishwa siku ya Alhamisi, wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin alikiri kwamba Urusi inahitaji kuimarisha ulinzi wake wa anga kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kremlin ilibainisha kwamba Rais Putin alikuwa bado hajaiona barua hiyo lakini kwamba Volodymyr Zelensky anaweza kuja kukutana naye “wakati wowote” huko Moscow, uwezekano ambao rais wa Ukraine anakataa katika barua yake. “Ukraine inapendekeza kukomesha vita hivi kupitia mawasiliano ya moja kwa moja kati yako na sisi. Ninapendekeza mkutano,” ameandika Volodymyr Zelensky, akipendekeza “Uswisi, Uturuki, na nchi za ulimwengu wa Kiarabu.” Ameongeza kuwa Ukraine iko “tayari kwa ajili ya kusitisha mapigano kamili kwa muda wote wa mazungumzo,” ambapo anabaini Ulaya na Marekani lazima zishiriki.
Mkutano kati ya viongozi hao wawili utakuwa “mzuri,” amesema Rais wa Marekani Donald Trump, akibaiisha kwamba Urusi na Ukraine zitalazimika “kukubaliana.”
Barua ya Volodymyr Zelensky ilichapishwa siku moja baada ya ndege zisizo na rubani za Ukraine kushambulia kituo cha mafuta na kambi ya wanamaji huko Saint Petersburg, mji wa Vladimir Putin, ambapo Jukwaa la Kiuchumi la Kimataifa la St. Petersburg (SPIEF) la kitamaduni lilikuwa likianza.
Mazungumzo yasitishwa
Rais wa Ukraine mara chache amezungumza moja kwa moja na mwenzake wa Urusi tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 2022, lakini ameitisha mkutano mara kwa mara, akibaini kwamba ni mkutano wa ana kwa ana pekee ndio unaweza kufikia makubaliano.
Juhudi za mazungumzo chini ya upatanishi wa Marekani zimesitishwa tangu mwanzo wa vita katika Mashariki ya Kati. Moscow inadai makubaliano ya kisiasa na ya kimaeneo kutoka Kyiv, ikiwa ni pamoja na kujiondoa kabisa kutoka eneo la Donetsk, ambalo linadhibitiwa kwa kiasi fulani na Moscow. Ukraine inapinga madai haya, ikiyaona kama kujisalimisha.
Kyiv pia imependekeza mara kwa mara kusitisha mapigano kwa muda mrefu ili kurahisisha mazungumzo. Lakini Moscow inakataa wazo hili, ikisema kwamba lingeruhusu jeshi la Ukraine kujiimarisha. Rais wa Urusi alihoji tena uhalali wa mwenzake wa Ukraine kufanya mazungumzo, akibainisha siku ya Alhamisi kwamba muhula wa Volodymyr Zelensky ulimalizika mwaka wa 2024. Chini ya sheria za kijeshi, tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, hakuna uchaguzi unaoweza kufanyika.