
Iikiwa ni katika kunufaika na haki yake ya kujilinda na kujibu ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji vita na jinai za kinyama zinazofanywa na utawala dhalimu wa Israel dhidi ya watu wa Lebanon, vikosi vya jeshi la Iran Jumapili usiku vilitoa jibu kali la makombora katika maeneo ya utawala huo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Maeneo yaliyolengwa katika shambulio hilo kubwa la makombora kimsingi ni ya kijeshi na kistratijia ya utawala wa Israel.
Operesheni hii ya kuiadhibu Israel imefanyika baada ya utawala huo wa Kizayuni kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, kukiuka mara kwa mara usitishaji vita katika ardhi ya Lebanon, ambapo umekuwa ikishambulia kiholela maeneo ya kusini mwa nchi hiyo na vitongoji vyake na kuua kinyama makumi ya raia wasio na hatia.
Katika kukabiliana na jinai kubwa za utawala ghasibu wa Israel huko kusini mwa Lebanon na kuenea mauaji ya raia pamoja na kuhamishwa kwa nguvu wakazi madhulumu wa maeneo ya Sour na Nabatieh na maeneo mengine ya nchi hiyo, vikiwemo vitongoji vya mji mkuu Beirut, Kambi ya Anga ya Ramat David, ambako mashambulizi hayo ya kinyama ya Wazayuni yamekuwa yakipangwa na kutekelezewa, imelengwa kwa makombora ya balistiki ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kukubali Iran usitishaji vita wa tarehe 10 Aprili kulitimia kwa masharti ya usitishaji mapigano katika medani zote za vita na hasa nchini Lebanon; lakini pamoja na hayo, na kama ilivyo kawaida yazo, Marekani na utawala wa Kizayuni hazikutekeleza ahadi zao, na hivyo kuendeleza uchokozi na jinai zao huko Lebanon. Ukiukaji vita huo umekuwa ikitimia kwa kushambuliwa mara kwa mara maeneo ya pwani na meli za Iran katika Lango-Bahari la Hormuz, Bahari ya Oman na Bahari ya Hindi na vilevile mashambulio ya utawala haramu wa Israel katika ardhi ya Lebanon.
Kwa hivyo operesheni ya Jumapili usiku ilikuwa onyo la awali, na ikiwa uchokozi huo utaendelea kukaririwa, majibu ya Iran yatakuwa makubwa na makali zaidi na yatajumuisha shabaha zote za Wamarekani na Wazayuni katika eneo hili nyeti la Mashariki ya Kati.
Itakumbukwa kuwa baada ya vita vya siku 40 vya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, utawala wa Kizayuni na Marekani, usitishaji vita ulianzishwa kwa upatanishi wa Pakistan katika mazungumzo ya mjini Islamabad. Moja ya masharti muhimu, ya wazi na yasiyojadiliwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mapatano hayo lilikuwa kusimamishwa usitishaji vita kikamilifu katika ngome na medani zote za vita ikiwemo Lebanon na vilevile kusitishwa mara moja hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu madhulumu wa Lebanon. Ikumbukwe kuwa baadhi ya makundi na nchi zinazoshirikiana na Marekani na Wazayuni katika eneo zilikuwa zimeanzisha propaganda na uchochezi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kudai kinyume na ukweli kwamba, Iran ilikuwa imewasaliti washirika wake kwa kutowatetea na kuwaacha washambuliwe kinyama na Wazayuni kwa ushirikiano wa Marekani. Nchi na makundi hayo ya kichochezi yalifasiri vibaya na kwa makusudi subira ya Iran kuhusiana na jambo hilo na kujaribu kuwakatisha tamaa watu wa Lebanon kwa kueneza uvumi usio na msing dhidi ya Iran. Lakini sasa baada ya Iran kutoa jibu hilo kali kwa uchokozi na jinai za Israel nchini Lebanon, wachochezi hao wamenyamaza kimya kwa sasa lakini bila shaka wataendelea kutafuta visingizio vingine vya kuipaka matope Iran na washirika wake wa mrengo wa muqawama katika eneo, ikiwa ni katika kuendelea kuhudumia maslahi ya maadui wa Uislamu.
Utawala wa Kizayuni kwa uungaji mkono wa wazi wa Marekani na hasa utawala wa hivi sasa wa Donald Trump, umekuwa ukikiuka hadharani sheria za kimataifa pamoja na makubaliano ya usitishaji vita bila kujali lolote, ambapo umekuwa ikitekeleza bila huruma mauaji ya halaiki na jinai za kutisha dhidi ya raia wa kawaida katika Ukanda wa Gaza na kusini mwa Lebanon. Bila shaka ukiukaji huu wa mara kwa mara wa sheria na mikataba ya kimataifa ni ishara ya wazi ya kuendelea kwa siasa zake za kigaidi na kijinai dhidi ya mataifa ya eneo.
Viongozi wa Iran wamekuwa wakisema mara kwa mara kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitabakia kimya mbele ya ukiukaji wowote wa usitishaji vita, hususan katika upande wa Lebanon, ambalo lilikuwa moja ya masharti makuu ya makubaliano ya Islamabad. Jibu la makombora la usiku wa Jumapili ni sehemu tu ya gharama ambayo wavamizi wanapaswa kuilipa.