Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini imefanikiwa kuokoa milioni 69,248,392 kupitia opareshen maalum katika kukusanya fedha za serikali ambazo zimechelewesha benki na mashine za posi.
Akizungumza na waandishi wa Habari Naibu Mkuu wa TAKUKURU amesema baada ya Oparesheni hiyo kwa kushirikiana na manispaa ya Morogoro, TAKUKURU imegundua kuna ucheleweshaji wa fedha benki, udhaifu wa mifumo ya Tehama pamoja na kukaa na fedha za serikali muda mrefu hivyo kusababisha kupotea kwa fedha za makusanyo.
Aidha TAKUKURU kutokana na jitihada zinazoendelea katika kupambana na Rushwa TAKUKURU Morogoro imeanzisha klabu za kupinga Rushwa katika vikundi maalum na itaendelea kutoa elimu ya rushwa kwenye vyombo mbalimbali
vya habari.
(Feed generated with FetchRSS)