
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeripoti kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hii vimetoa vipigo vikali kwa kambi za Marekani na mali mbalimbali katika kanda hii ambavyo Marekani imevitumia kuishambulia Iran.
Muendelezo wa hujuma dhidi ya Iran ulishtadi mapema leo Jumatano, wakati Marekani ilipofanya “mashambulizi makali” kwenye maeneo ya kusini mwa Iran kwa kisingizio kwamba moja ya helikopta zake aina ya Apache ilianguka kwenye Mlango Bahari wa Hormuz Jumanne usiku.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema: Mashambulizi ya Marekani yanakiuka waziwazi Mkataba wa Umoja jwa Mataifa hasa kifungu cha 2, kipengee cha 4 na kanuni msingi inayokataza matumizi ya nguvu katika mahusiano ya kimataifa.
Kwa vitendo hivi vya uchokozi, serikali ya Marekani kwa mara nyingine imedhihirisha asili yake ya uhalifu na mienendo ya uchochezi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema: Katika kujibu hujuma za kijeshi na ukukiukwa mamlaka ya kujitawala nan umoja wa ardhi nzima ya Iran vikosi shupavu vya ulinzi vya nchi hii vimezishambulia kambi za Marekani na mali nyinginezo katika eneo ambazo zimetumiwa kutekelezea mashambulizi dhidi ya Iran.
Imeongeza kuwa: Mashambulio hayo yamefanywa ili kutekeleza “haki ya asili ya Iran ya kujilinda,” kufuatia tangazo la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC kwamba lilikuwa limeashambulia kwa makombora ya fueli mango ya masafa marefu maeneo manne muhimu ya Marekani huko Al-Azraq Jordan na kuharibu hangari ya ndege za kivita za F-35.
Saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo pia, Jeshi la Wanamaji la IRGC lilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Wanamaji cha jesi la Marekani nchini Bahrain na katika kambi ya jeshi la Marekani ya Ali al Salem huko Kuwait.